HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 23, 2016

PRIDE Tanzania Yatoa Misaada mbalimbali kwa wateja wake ambao ni waathirika wa tetemeko la Ardhi Bukoba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Mstaafu,Salum Kijuu (katikati) akiwa katika picha ya pampja na Uongozi wa PRIDE Tanzania, ulioongozwa na Meneja wake wa Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo (wa tatu kulia) baada ya zoezi la upokeaji wa misaada mbalimbali kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi katibuni. Wengine ni Meneja wa PRIDE tawi la Bukoba, Afisa wa PRIDE tawi la Bukoba pamoja na viongozi wa wateja wa PRIDE tawi la Bukoba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu akimshukuru Meneja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba Bi. Digna Tarimo baada ya kupokea msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
Meneja wa Pride Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Mstaafu, msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
Afisa wa PRIDE Tanzania, Ndugu Samson Tenga akifanya tathmini kabla ya kumkabidhi Mteja wa PRIDE Tanzania, Tawi la Bukoba mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake ambayo ilibomoka kutokana na janga la tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni.
Diwani wa Kata ya Miembeni, Manispaa ya Bukoba, Mkoa wa Kagera (Shati la Kijani) Bw. Richard Gaspar pamoja na maafisa wa PRIDE Tanzania wakimkabidhi mifuko ya saruji mteja wa PRIDE, ambaye nyumba yake iliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba. 

PRIDE ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) linalotoa huduma za kifedha kwa masharti nafuu kwa wafanya biashara ndogondogo na wa kati. Huduma hizo zina lengo la kuchangia pato la taifa na kuondoa umasikini nchini.

PRIDE ilisajiliwa mnamo Mei 1993 chini ya wadhamini wasio na hisa (Company Limited by guarantee, not Having Share Capital) kulingana na Sheria ya Makampuni Cap, 212 ya mwaka 2012. na kuanza rasmi shughuli zake mwaka 1994 mjini Arusha. Kwa sasa Shirika lina matawi 85 yalioenea nchini nzima.

Tangu kuanzishwa, PRIDE imeweza kukopesha wajasiliamali mbalimbali nchini wapatao 1,700,000 na kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni mia tisa (bil. 900.0).

Katika kuungana na Watanzania, PRIDE Tanzania walitoa misaada mbalimbali moja kwa moja kwa wateja wao wa tawi la Bukoba ambao waliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera. Msaada huu ulilenga kuwawezesha wateja wa PRIDE kukarabati makazi yao.

Vilevile PRIDE ilichangia katika mfuko wa maafa wa serikali kwa kutoa mifuko ya saruji na mabati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad