Balozi wa Ujerumani hapa nchini – Egon Kochanke (katikati) na Ofisa kutoka Ubalozi huo, Julia Hannig (kushoto), wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), alipokuwa akifafanua jambo walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kufanya mazungumzo naye kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika sekta ya nishati.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), akitazama kabrasha alilopatiwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke (katikati), linaloonesha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika sekta ya nishati. Kushoto ni Ofisa kutoka Ubalozi huo, Julia Hannig. Balozi Kochanke alimtembelea Waziri Muhongo hivi karibuni ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Balozi wa Ujerumani hapa nchini – Egon Kochanke, Waziri wa Nishati na Madini – Profesa Sospeter Muhongo na Ofisa kutoka Ubalozini – Julia Hannig, wakiwa katika picha ya pamoja ofisini kwa Waziri Muhongo mara baada ya mazungumzo ambayo yalifanyika ofisini hapo hivi karibuni kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, hususan katika sekta ya nishati.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Kochanke baada ya mazungumzo yao. Balozi Kochanke alimtembelea Waziri Muhongo hivi karibuni Ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuzungumzia ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika sekta ya nishati.


No comments:
Post a Comment