Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya DCB Edmund Mkwawa akizungumza na wanachama wa mfuko wa wafanyakazi wa benki hiyo mwishoni mwa wiki hii wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka saba toka kuanzishwa.
Katibu Mkuu wa mfuko wa wafanyakazi wa DCB, Maridha Nassor akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka saba toka kuanzishwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya DCB Edmund Mkwawa akikata keki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka saba toka kuanzishwa.
wafanyakazi wa DCB wakiwa katika hafla ya kuadhimisha miaka saba toka kuanzishwa.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya DCB Edmund Mkwawa amechangia kiasi cha milioni tano kwenye mfuko wa wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa kusherrhrka miaka saba toka kuanzishwa kwao.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wili, Mkwawa amesema kuwa anawapa pongezi kubwa sana wafanyakazi kwa juhudi kubwa walizozifanya za kuwa na mfuko wao unaoiwasaida wao wenyewe na menejimenti ya DCB ina wajibu wa kuhamasisha zaidi kwa wanachama kujiunga.
Mkwawa amesema, kwa sasa mfuko huo una wafanyakazi kutoka matawi mbalimbali ya benki hiyo na hiyo nu moja ya hatua kubwa waliyofikia kuhakikisha na kuwa na mfuko wao wenyewe wenye malengo mazuri na kusaidiana wakati wa shida na raha.
Katibu Mkuu wa mfuko huo wa wafanyakazi wa DCB, Maridha Nassor amesema kuwa mfuko huu ulianzishwa kwa lengo la kusaidiana na kumnfariji mwanachama pale anapokuwa na matatizo ikiwemo kufiwa.
Maridha amesema kuwa mfuko huo ulianza na wanachama 25 wote wakiwa kutoka tawi la Magomeni lakini kwa sasa wsapo watu 57 huku wengine wakiwa wamehama kwenye matawi mengine pia.
No comments:
Post a Comment