HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 16, 2016

HAWA NDIO WASANII WA BONGO FLEVA WALIOTOA NYIMBO NA WAPENZI WAO HIVI KARIBUNI

Katika siku za hivi karibuni wasanii wengi wa bongo fleva wametoa nyimbo wakiwa na wapenzi au aidha kwa kuimba pamoja nao au kwa kuwatumia kama warembo (video queen) katika video zao.
 
Hadi sasa kuna wasanii wanne wa bongo flava ambao tayari video za nyimbo zao zimeshatoka na wakionekana na wapenzi wao katika video hizo.

Mwanamuziki Young Dee a.k.a Pakarapper yeye ndiye alikwa wa kwanza kudondosha kichupa cha wimbo wake wa furaha ambapo ndani ya video ya wimbo huo, mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Tunda ndiye mrembo wa video (video queen).
Baada ya Young Dee alifuata Vanessa Mdee na Jux ambapo wiki moja sasa imepita tangu walipotoa video ya wimbo wao Juu. Wimbo huu wameimbiana wao wenyewe wakielezeana na kwa kiasi gani wanapendana na kila mmoja atakavyoumia ikitokea mwenzake hayupo naye tena.
Siku moja iliyopita mwanamuziki Judith Wambura a.k.a Lady JayDee na mpenzi wake Spicy wameachia video ya wimbo wao unaofahamika kwa jina la Together Remix. Wimbo huu ni maboresho ya wimbo wa Lady JayDee unaoitwa Together.
Wanaotufungia ukurasa wetu kwa leo ni wasanii wawili wanaounda kundi la The Amazing ambapo pia wanauhusiano. Hapa namzungumzia Izzo Bizness na Abela Music ambao jana wameachia video ya wimbo wao unaoitwa Umeniweza. CHANZO: SWAHILITIMES

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad