Na Zaina Nyamka, Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Serengeti Boys kikiwa katika mazoezi ya kujenga utimamu wa mwili chini ya Mshauri wa benchi la ufundi Mholanzi Kim Poulsen na kocha Mkuu Bakari shime katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam leo.
Timu hiyo imeingia kambini jana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu kucheza kombe la mataifa Afrika nchini Madagascar 2017 chini ya umri wa miaka 17 dhidi ya Visiwa vya shelisheli Juni 26 mechi itakayopigwa kwenye dimba la uwanja wa Taifa.
Kocha Mkuu Bakari shime wa kikosi cha timu ya Serengeti Boys wakifanya mazoeti ya kuweka utimamu mwili katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam leo.

Mshauri wa benchi la ufundi Mholanzi Kim Poulsen katika akiwasimamia wachezaji wa kikosi cha Serengeti Boys kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu kucheza kombe la mataifa Afrika kwa vijana wa umri wa chini ya Miaka 17 nchini Madagascar 2017 dhidi ya Visiwa vya shelisheli Juni 26 mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment