Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linawashikilia watu 13 kwa kitendo cha kuuza sukari kinyume na bei ilekezi iliyopangwa na serekali ya shilingi 1800.
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo Alisema kuwa watu hao wamekamatwa katika maduka tofauti tofauti kufuatia operesheni kabambe iliyoandaliwa na jeshi hilo kwa ajili ya wafanyabiashara wote ambao wanauza sukari bei ya juu pamoja na walioficha sukari.
Alisema kuwa kumekuwa na wafanyabiashara ambao wamejipandishia bidhaa hii ya sukari na kuuza bei ambayo wanaitaka wenyewe badala ya kuuza bei ambayo imepangwa na serekali ambayo ni shilling 1800.

"kuna wafanya bishara wameamua kujichukulia sheria mkononi na kuanza kuuza sukari bei ghali huku wengine wakiwa wanaficha sukari ili isiwepo madukani na wapandishe bei, jambo ambalo sio zuri ndugu waandishi tumewakamata wafanyabiashara 13 hadi sasa ambao walikuwa wamejipandishia bei kiholela holela na wengine wanauza sukari hadi shilingi 5500 kwa kilo, wengine 4500 huku wengine wakiwa wanauza 3000 kitu ambacho sio cha haki na ni kinyume na sheria" alisema Mkumbo.
Aidha aliwataja baadhi ya wafanyabishara ambao wanashikiliwa na jeshi la hilo kuwa ni pamoja na mmiliki wa Rafiki Mini super market aliyejulikana kwa jina la James Wiliam ambaye yeye aliuza sukari kilo moja kwa shilingi 5500, Pick pay supermarket ambeye yeye aliuza sukari kilo moja kwa shilingi 3000, Sayana Grokoli ambayo inamilikiwa na Muhidin Kitibwi ambaye yeye aliuza sukari kilomoja kwa shilingi 5000 pamoja na mama Anna Silayo ambaye yeye aliuza sukari kilimoja kwa shilingi 3000 huku Muhame Suhaul ambaye yeye alikuwa anauza sukari kilo moja kwa shilingi 6200.
Alisema kuwa watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani na sheria itafata mkondo wake na watashitakiwa kwa kosa la kuhujumu uchumi wa nchi.
Alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha hususani wafanyabiashara kuuza sukari kwa bei elekezi iliotolewa na serikali na sio kujipandishia bei kiholela holela huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa mfanyabiashara yeyote ambaye atakuwa anauza sukari kinyume na taratibu na yule ambaye atakuwa amehifadhi sukari nyingi katika ghala au sehemu yeyote.
Mkumbo alimalizia kwa kusema zoezi hili halitaishia hapa ni endelevu na wataendelea kufuatilia kila kona kubaini watu ambao wanakiuka sheria.
Mtandao huu ulibahatika pia kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha nao waliomba serikali iwafatilie wafanyabishara hao wa maduka ambao wanauza sukari kwani wanajipandishia bei kiholela hali ambayo inawafanya wanachi wengine kushindwa kunywa chai asubui kutokana na kutoweza kununua sukari kwa bei ya juu.

No comments:
Post a Comment