HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 22, 2016

Programu ya 'Seeds for the Future' nchini Tanzania yazinduliwa na Huawei.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang akisoma hotuba yake kwa wageni waalikwa wakati wa halfla ya uzinduzi wa programu ya elimu inayoitwa “Seeds for the Future” nchini Tanzania. Programu hiyo ambayo inatoa nafasi 10 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei iliyopo Shenzhen, China ilizinduliwa rasmi mjini Dodoma mwishoni mwa juma.
 Meneja Uhusiano wa Huawei Tanzania Bw. Jimmy Liguo akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) kuhusiana na programu ya “Seeds for the future” wakati wa uzinduzi rasmi wa programu hiyo uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma. Kupitia programu hiyo Huawei imejitolea kudhamini mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi 10 wa vyuo vikuu hapa nchini kila mwaka kwa kipindi cha miaka 10.
  Mgeni rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Tanzania Prof. Simon Msanjila kushoto) akisikiliza hotuba mbalimbali za wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa programu ya Huawei “Seeds for the future” ambayo inatoa nafasi 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 10 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China ambapo wataweza kujipatia ujuzi. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma. (Katikati) ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Zanzibar Mhe. Abdullah Mzee na (Kulia) ni Mkuu wa Idara ya TEHAMA katika Chuo kikuu cha Dar es salaam Dk. Musa Kisaka.
 Mgeni rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Tanzania Prof. Simon Msanjila (katikati) akipeana mkono na mwakilishi wa Ubalozi wa China hapa nchini Lv. YouQing mara baada ya kuzindua rasmi programu ya Huawei”Seeds for the future” ambayo inatoa nafasi 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 10 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma. (Kulia) ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Zanzibar Mhe. Abdullah Mzee.

Wageni wa Meza kuu na baadhi ya wafanyakazi wa Huawei wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi 10 wa vyuo vikuu nchini ambao kupitia programu ya “Seeds for the Future” inayodhaminiwa na Huawei walichaguliwa kwenda China kujifunza na kufanya kazi na kampuni hiyo yenye makao makuu yake Shenzhen, China. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma.

KAMPUNI ya Huawei inayoongoza kwenye utoaji wa huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ulimwenguni, leo imezindua programu ya elimu inayoitwa Seeds for the Future hapa nchini Tanzania.
 
Programu ya ‘Seeds for the Future’ inatoa nafasi 10 kwa wanafunzi wa hapa nchini kutoka vyuo vikuu kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China.
 
Mradi huo umelenga kuwa kusaidia kile kinachofundishwa shuleni kukidhi mahitaji halisi ya soko la ajira kwa vijana hapa nchini ikiwa ni pamoja na kupanua uelewa wa TEHAMA na kuhamasisha ushiriki katika sekta hii ili kuendana na  jamii ya sasa teknolojia ya habari na mawasilino.
 
Akizunguma wakati wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliochaguliwa kusoma China, Mkurugeni Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Bruce Zhang alisema ni wazi kwamba wanafunzi hawa watapewa kipaumbele kwenye fursa za kujifunza kupitia kujumuika na wafanyakazi wa Huawei na kutembelea maabara ya kampuni hiyo ambako wataweza kuona na kufanya majaribio ya teknolojia ya hali ya juu ya mawasiliano.
 
Alisema vijana hao watapa ujuzi wa kisasa unaowawezesha kushindana katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano, huku wakijufunza kukabiliana na ushindani katika soko la ajira.
 
 “Uzinduzi wa mpango huu inathibitisha kuwa tutaendelea kusaidia sekta ya TEHAMA hapa nchini,” alisema mkurugenzi huyo.
 
“Kupitia ushirikiano huu na Huawei, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Ninaamini wanafunzi hawa watakuwa na fursa ya kipekee kufanya kazi na kusoma makao makuu ya Huawei, huku wakijifunza utamaduni wa China na kutembelea maeneo muhimu ya vivutio vya utalii,” alisema Bruce
 
Alisema, mradi huu unafanyika kwenye nchi mbalimbali ulimwenguni ambako Kampuni ya Huawei inafanya shughuli zake na hapa nchini mpango umeshaandaliwa kwa wanafunzi 10 ambao watashiriki programu hii China na watasafiri tarehe 20 Mei mpaka  3 Juni ambapo watashiriki mafunzo hayo muhimu.
 
 
Alisema, ‘Seeds for the Future’ ni jambo linalodhihirisha kwamba Huawei imeweka mkazo katika maendeleo ya elimu ya TEHAMA vyuo vikuu kama jinsi ilivyojidhihirisha wakati wa kuzindua mradi huu wa elimu.”
 
Naye Mgeni rasmi wa shughuli hiyo ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Profesa Simon Msanjila alisema kuanzishwa kwa programu hii ni ushahidi kwamba Kampuni ya Huawei imedhamiria kusaidia maendeleo ya TEHAMA katika vyuo vikuu nchini pamoja na kuifanya Tanzania kung’ara katika teknolojia ya habari na mawasiliano.
 
 “Hii itawawezesha wanafunzi wetu kujifunza kwa kuelewa na kuwaandaa kuwa wafanyakazi mahiri kwenye masuala ya IT na sekta ya mawasilino,” alisema Profesa Msanjila.
 
.
Naibu Katibu huyo wa Elimu aliongeza kwamba; “Programu ya Seeds for the Future itawasaidia wanafunzi kutoka vyuo hivyo viwili kujifunza mambo mengi ili kuendana na mahitaji ya soko la dunia kwenye TEHAMA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad