Mgeni rasmi alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga. Maadhimisho hayo yameanza kwa maandamano kupitia maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kisha kumalizika kwa mkutano katika viwanja vya Shycom. YWCA ni shirika lisilo la kiserikali linatoa huduma kwa wanachama na wasio wanachama bila kujali utaifa,jinsia au imani ya mtu.
Lengo la shirika hilo ni kuunganisha uongozi na sauti za wanawake na wasichana ili kujenga usawa wa kijinsia,kiuchumi,kudumisha amani na uhuru sambamba na kutunza mazingira ya ustawi wa jamii yote. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kidunia ni "Kuunda Ulimwengu Unaojumuisha Wote" huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo kanda ya ziwa ikiwa ni "Kwa Pamoja Tuzuie Ndoa na Mimba za Utotoni,Tutaleta Mabadiliko Kielimu".
Washiriki wa maadhimisho hayo walisisitiza umuhimuwa jamii kuungana kwa pamoja ili kupiga vita mimba na ndoa za utotoni kwani janga kubwa sana katika kanda ya ziwa na hasa katika mkoa wa Shinyanga ambao unaongoza kitaifa kwa asilimia 59 ukifuatiwa na mkoa wa Tabora na Mara.
Akizungumza katika maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro alikemea tabia ya wazazi na walezi kuwapa "Samba" Watoto wa Kike "Dawa ya kusafisha nyota watoto wa kike ili wapendwe na wanaume" hali inayochangia watoto kupewa mimba wangali wadogo matokeo yake kubaki wanalalamika wakati wao ndiyo chanzo cha matatizo.
Matiro aliagiza waganga wa jadi na wazazi wanaowapa "Samba" watoto wao wakamatwe kwani wanaharibu watoto na kusababisha tatizo la mimba na ndoa za utotoni kuendelea kuwepo katika jamii.
Katibu wa YWCA mkoa wa Shinyanga Maryciana Makundi akizungumza wakati wa maadhimisho hayo katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambapo alisema YWCA Tanzania ilianzishwamwaka 1959 ikiwa ni miongoni mwa nchi 125 duniani zinazounganishwa na World YWCA ambayo makao yake makuu yapo Geneva Uswis.
Alisema maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka mwezi Aprili yakiwa na lengo la kujenga jamii yenye kuheshimu utu wa binadamu,kutetea na kulindaa haki,usawa na amani kwa wote
AKC kwaya kutoka Kanisa la Kambarage wakitoa burudani
AKC Kwaya wakitoa burudani
Kulia ni Katibu mkuu wa YWCA Tanzania Louisa Bulemela akitoa historia ya shirika hilo na jinsi linavyofanya kazi zake nchini.Alisema shirika hilo lina matawi 21 katika mikoa 11 nchini Tanzania,likiwa na wanachama zaidi ya 2000 wengi wao wakiwa ni akina mama na vijana
Wanachama wa YWCA wakiwa eneo la tukio

No comments:
Post a Comment