HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 18, 2016

DUKA JIPYA LA VODACOM LAFUNGULIWA MBEYA.

 Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya, David Mwashilindi akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa duka la Vodacom Tanzania lililopo Mwanjelwa Mkoani humo,Anayeshuhudia ni Meneja wa Mauzo wa kampuni hiyo,Emanuel Sagenge.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Lusajo Benson (kushoto) akimpatia maelezo Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Mch. David Mwashilindi,mara baada ya kuzindua duka la Vodacom Tanzania lililopo Mwanjelwa Mkoani humo jana.
 Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya, David Mwashilindi, akikata keki maalumu ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa duka la Vodacom Tanzania lililopo Mwanjelwa Mkoani humo hapo jana,Wengine katika picha ni wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja(kulia)
Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Mch. David Mwashilindi,akimlisha keki Robert Mwakisika ambaye alikuwa mteja wa kwanza kupata huduma katika duka jipya la Vodacom Tanzania,lililopo Mwanjelwa Mkoani Mbeya mara baada ya kilizindua hapo jana.

 *Ni duka la 100 kufunguliwa nchini.
Katika mkakati wake wa kusogeza  huduma zake karibu na wananchi,kampuni ya Vodacom mwishoni mwa wiki imefungua duka jipya mkoani Mbeya. Duka hili ni la 100 kufunguliwa nchini na la tatu kufunguliwa mkoani Mbeya.

Kufunguliwa kwa  duka hili kutawawezesha wateja wa Vodacom kupata huduma za kampuni kwa karibu ambapo pia kampuni itafungua vituo vya huduma kwa wateja vipatavyo 300 sehemu mbalimbali  chini ikiwemo mkoani humo katika siku za karibuni.

Huduma mbalimbali zinapatikana katika duka hilo ikiwemo huduma za kutuma na kupokea fedha ya M-Pesa,kusajili laini za wateja,kuunganisha  wateja kwenye mtandao na kuuza simu na vifaa vingine vya mawasiliano.
“Ufunguzi wa duka hili la Mwanjelwa ni mkakati wa kuimarisha na kuboresha huduma zetu na kuwa karibu na wateja.Hivi sasa wateja wanaweza wakapata huduma zetu wakati wowote ndani ya masaa 24 kupitia simu ya huduma kwa wateja na tunawaahidi wateja wetu kuendelea kuwapa huduma bora na kuwasikiliza”,Alisema  Mkuu  wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyasa-Mbeya, MacFadyne Minja.

Akiongea katika uzinduzi huo,mgeni rasmi Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya, David Mwashilindi alisema Vodacom kwa kuzidi kusogeza huduma za mawasiliano  kwa wananchi mkoani humo kwa kuwa na mawasiliano bora yanachochea kukua kwa uchumi na maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.

“Nawapongeza kwa kusogeza huduma zenu karibu na wananchi,nimeambiwa kuwa mnao wateja zaidi ya 1,000 mkoani hapa,kuzidi kuwasogezea huduma ni jambo zuri ambalo litawawezesha kuokoa muda waliokuwa wanatumia kufuata huduma zenu mbali”,Alisema Mwashilindi.

Mbali na duka la Mwanjelwa lililofunguliwa leo kampuni ya Vodacom inatarajia katika siku za usoni kufungua maduka yake katika maeneo ya vyuo vya elimu ya juu vya  St.John, Mbeya University of Science and Technology na  Mbalizi Institute of Health Sciences.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad