Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka, ( DART) imetaka elimu kwa umma juu ya matumizi za miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kuwa ni kipaumbele kabla ya mabasi hayo kuanza kazi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya wadau wa karibu ya kukagua miundombinu na alama za barabarani ili matumizi yake yawe sahihi, Meneja wa Usimamizi Miundombinu wa Wakala, Mhandisi Mohamed Kuganda, amesema elimu ndiyo italinda miundombinu, usalama wa watumiaji na kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwa kila upande.
“Elimu ni muhimu kwa mafanikio ya mradi. Watumiaji wakifanya mambo sahihi miundombinu itakuwa salama na hawatopata usumbufu wa aina yoyote. Tulichokifanya leo tumechukua watu wa karibu wanaohusika na mambo ya usafirishaji, ili tuweze kuelimishana kwa pamoja na elimu hii tutaisambaza kwa umma, hasa watu wanaoendesha vyombo barabarani,”
Katika ziara hiyo walikuwemo maofisa wa DART, Polisi Usalama Barabarani, Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) na Mshauri Elekezi (SMEC). Ukaguzi, ambao unafanywa kwa awamu, ulianzia kituo cha Kimara hadi Morocco.
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi ( SSP ), Awadhi Jihad, ambaye ni Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, alisema jeshi la polisi litazifanyia kazi changamoto zilizojitokeza.
“Kazi yetu ni kusimamia sheria na kanuni za Usalama Barabarani. Tumejifunza mambo mengi na bado tutaendelea kujifunza kwa kuwa miundombinu hii ina mabo mengi ambayo hayamo katika barabara za kawaida.”
Bw Awadhi alisema alama zipo nyingi sana katika mradi huu, hivyo watumiaji wanatakiwa kuwa makini, ili kuepuka kufanya makosa,” na kuahidi kwamba polisi wa usalama barabara watajitahidi kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara hasa madereva hata baada ya mradi kaanza kufanya kazi.
Bw Awadhi ameonya kwamba madereva wa magari, pikipiki, maguta na wanaotumia miundombinu na kuvunja sheria kwa makusudi watachukuliwa hatu kali za kisheria.
“Hawa watu tutawapiga faini kama sheria inavyosema lakini ikibidi tutawafikisha mahakamani kwa sababu wanafanya kusudi,” alisisitiza.

No comments:
Post a Comment