Mkurugenzi wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Agrey Mlimka akiwa anafafanua jambo katika mkutano wa siku moja wa kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili waajiri mkutano uliowashirikisha waajiri kutoka katika sekta mbalimbali uliofanyika ndani ya hotel ya Kibo palace jijini Arusha leo
wanachama wa chama cha waajiri pamoja na wasio wanachama wa wakiwa wanajadili kwa makini changamoto ambazo zinawakabili waajiri na jinsi ya kuzitatua .
Na Woinde Shizza,Arusha
Chama cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa vikwazo katika biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya rushwa pamoja na urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa na kimataifa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri (ATE),Aggrey Mlimuka akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri amesema kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa nafasi za ajira ili kujenga uchumi endelevu wa nchi
Mkurugenzi huyo ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu kutoka nje kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na kupunguza tozo kubwa za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia 5%.
Kwa upande wake Afisa Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipata adha kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya nchi suala ambalo serikali inatambua kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu kutoka nje.
No comments:
Post a Comment