Mabondia Mada Maugo (kushoto) na Abdallah Pazi wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam. katikati ni Mratibu wa Mpambano huo kocha wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D'.
Mratibu wa mpambano wa masumbwi, Rajabu Mhamila 'Super D' (katikati) akiwa na mabondia Mada Maugo (kushoto) na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.
Bondia Mada Maugo akikabidhiwa mkataba wake na mratibu wa mpambano wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kati yake na Abdallah Pazi mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Bondia Abdallah Pazi kushoto akipokea mkataba wake kutoka kwa mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kusaini kwa ajili ya kupigana na Mada Maugo siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa. Picha na SUPER D BOXING NEWS
No comments:
Post a Comment