HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 2, 2016

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ATUA MACHINJIO YA VINGUNGUTI USIKU, AKUTANA NA MADUDU YA KUTAFUNA KODI

Katika hatua ya kushitukiza,Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amefanya ukaguzi wa Machinjio ya Vingunguti usiku wa Ijumaa Januari 1, 2016.

Mh.Mwigulu Nchemba amefika kwenye Machinjio hayo usiku huo ilikushuhudia Mifugo ikiandaliwa kwa ajili ya kitoweo cha wananchi.Uchinjaji wa Ng'ombe na Mbuzi katika machinjio haya hufanyika nyakati za Usiku kuanzia saa 4 hadi 10 alfajiri.

Mbali na kusikiliza kero na maoni ya wananchi kuhusu uendeshwaji wa Machinjio hayo,Mwigulu Nchemba ameshuhudia utafunwaji wa kodi ya serikali inayokusanywa kwenye mnada wa Pugu.

Utafunwaji huo unatokana na uandikaji wa kibali cha mifugo michache kuja Machinjioni ili hali mifugo zaidi huingizwa machinjioni bila kibali.

Mathalani  Mh.Waziri ameshuhudia Ng'ombe waliotoka mnada wa Pugu ambao wameshalipiwa kodi wakiwa 1450 lakini kibali chake kimeandikwa Ng'ombe 300 tu.Ikimaanisha kuna ng'ombe 1150 wamelipiwa ushuru lakini machinjioni kimeletwa kibali cha ng'ombe 300 wakati kwa hesabu ng'ombe hao wanazidi 1000.

Kutokana na hali hiyo,Mh.Waziri ameagiza wahusika wote kufika kesho kwenye mkutano wa asubuhi kwa ajili ya hatua stahiki kuchukuliwa.
Mhe Mwigulu amesisitiza kuwa kwa mtu yeyote mwenye dhamana na kusimamia sekta ya kilimo,Mifugo na Uvuvi afanye kazi  kwa mujibu wa sharia,vinginevyo hakutakuwa na huruma kwa wanaohujumu.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akisikiliza kero za wadau wa machinjio ya Vingunguti usiku  wa January 01/01/2016.Mwigulu Nchemba akishuhudia Ng'ombe aliyetayari kwa taratibu za kuchinjwa kwa ajili ya kitoweo.
Mbuzi wakiwa tayari kwa ajili ya kuchinjwa kwenye machinjio hayo ya Vingunguti.Mbuzi hawa asilimia kubwa wanatoka mnada wa Pugu ambao Ushuru wake unakusanywa na serikali kuu.Waziri Mwigulu Nchemba akikagua maeneo ya machinjio hayo usiku huu.
Mwigulu Nchemba akitoa maagizo kwa uongozi wa Machinjio ya Vingunguti kukutana kesho saa 2:00 asubuhi kwa wahusika wote wenye dhamana na Machinjio hayo,Mkutano utafanyika eneo la Machinjio hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad