Watu
wengi wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda
kufanya utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za
Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii
wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa
fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa
mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa jiji.
Irente
View Point inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani
lushoto mkoani Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao
walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na
wengine walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada
hasa wakati wa sikukuu za Christmas
Eneo
hili lina urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza
kuona maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi
wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona
Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.
Hapa ndipo kileleni na Mwonekano wa Irente
Hii ni Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo hili kwa upande kwa Kushoto.
Eneo hili wakazi wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia picha
Hii ni njia ya kuelekea Pangoni
Ukiwa Juu ndani ya Pango utaona hivi
Mmoja wa wandishi wa Blogs za Mikoa Fredy Tony akiwa amefika kujionea eneo hilo.
(Imeandaliwa na Fredy A. Njeje 0765056399)
No comments:
Post a Comment