HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 26, 2015

WAZIRI MKUU KESHO KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI KIGOMA

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma
WAZIRI Mkuu Kassimu M Majaliwa(MB) (Pichani) kesho ataanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya alisema kuwa Waziri Mkuu atawasili Mkoani hapa kesho majira ya saa tatu asubuhi.

Alisema kuwa atapokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mkoa na kisha atasomewa taarifa ya Mkoa.

Baada ya hapo ataelekea katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo Wilayani Kasulu pamoja na kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo.


Na siku ya jumatatu atafungua mwalo wa kibirizi na kufanya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa NSSF na kisha kurejea Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad