HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 26, 2015

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI DAR ES SALAAM WANAWAKE 12 WAPATA WATOTO MKESHA WA KRISMAS

Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam Mwanne Satara akimsaidia kumuelekeza Lulu Mohamed namna ya kumfunika nguo Mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia Krismas Dar es Salaam ambapo akinamama 12 walipata watoto na Mmoja wa akinamama hao alipata mapacha 2 na kufanya watoto wa kiume kufikia 6 na wakike 7, kati yao akinamama waliofanyiwa upasuaji ni akinamama 10 na kati ya hao watoto njiti 2 na Hospitali ya Temeke akina mama waliojifungua hospitalini hapo kufikia idadi ya watoto 12, wakiume 4 na wakike 8 .
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
Afisa Muuguzi wa Zamu wa Hospita ya Mkoa Amana Florensia Ndumbaro akizungumza na waandishi wa Habari (pichani hawapo), Hospitali tumepokea idadi ya watoto waliozaliwa mkesha wa Krismas ni 33 kati yao 15 ni wakike na 18 ni wakiume na wote wapo katika hali nzuri na wananyonya vizuri pia mama zao wanaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad