Wakazi wa kijiji cha Olbolot , tarafa ya Goima katika kata ya Mrijo mkoani Dodoma wakumbwa na janga la mpasuko wa ardhi wa zaidi ya mita mia tano (500m) kutokana na mvua za mfululizo zinazoendelea kunyesha na kusababisha kaya zaidi ya 19 kukimbia makazi yao, picha ya kwanza inaonyesha Afisa Habari za Wakala a Jiolojia Tanzania (GST) Bw Samwel Mtuwa akihojiana na wananchi wa kijiji husika , picha inayofuata inaonyesha sehemu ya nyumba iliyoathiriwa na mpasuko, picha inayofuata ni watalaam kutoka GST wakifanya upimaji wa mpasuko ili kujua chanzo chake , na picha nyingine ni mkazi wa kijiji cha Olbolot akiangalia shimo kubwa katika shamba lake lililosababishwa na mpasuko. Pichani (kulia) ni watalaam kutoka GST wakifanya upimaji wa mpasuko ili kujua chanzo chak.
sehemu ya nyumba iliyoathiriwa na mpasuko. Picha na Samwel Mtuwa –GST, Dodoma.
No comments:
Post a Comment