HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 8, 2015

TAMASHA LA KUELEKEA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI LAFANYIKA LEO JIJINI DAR

 Mgeni rasmi katika Tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lililoandaliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation (DMF), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa kwenye meza kuu na Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Anna Mgwhira (kushoto), Mkurugenzi wa Hunduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila (kulia) pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel, wakati wa muendelezo wa tamasha hilo lenye lengo la kufanya harambee kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vifaa maalum vya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo. Kilele cha kumbukumbu hiyo ya mtoto njiti Duniani kinatarajiwa kufanyika Novemba 17, 2015.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika Tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lililoandaliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation (DMF), lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo. Akitoa hotuba yake, Makonda amesema kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ili kuhakikisha watoto njiti wanapata huduma stahiki katika mazingira rafiki ili waweze kuishi kama watoto wengine.
Mwenyekiti wa chama cha (ACT) Wazalendo, Anna Mgwhira ambaye alikuwa ni mmoja wa wageni waalikwa, akizungumza katika Tamasha hilo la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wa Hunduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila akizungumza katika hilo, lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akizungumza wakati akitoa shukrani kwa wadau mbali mbali waliolifanyikisha Tamasha hilo kwa namna moja ama nyingine.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondini, Paul Makonda akiteta jambo na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel katika tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani, lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondini, Paul Makonda akiagana na Mwenyekiti wa chama cha (ACT) Anna katika tamasha hilo. 
Sehem ya wadau mbali mbali na wananchi walio fika katika tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani leo katika viwanja vya Leaders Clubu jijini Dar es Salaam.
 Ankal Albert Makoye na Ankal Bosco Majaliwa pia walikuwepo kwenye Tamasha hilo.
Wadau kutoka taasisi ya Brigite Alfred Foundation pia walikuwepo kwenye Tamasha hilo la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnaba na Mwasit Almas wakishirikiana na The Voice wakitoa burudani katika Tamasha hilo la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.


Mgeni rami katika Tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lililoangaliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation (DMF), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akipatia maelezo kutoka kwa  baadhi ya wadau walioshiriki kutoa mafunzo katika Tamasha hilo.
Burudani ya kucheza na nyoka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad