Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei(kushoto)akimkabidhi Bw.Ajali Kibiki(kulia)cheti cha utendaji bora wa kutoa huduma nzuri kwa wateja katika duka la kampuni hiyo lililopo Makamba Mkoani Njombe,Wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kwa washirika wa kibiashiara.Wengine katika picha wapili toka kushoto ni Magreth Lawrence na Brigita Stephen.Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mshirika wa kibiashara wa Vodacom Tanzania,Moshi Kimila mkazi wa Kasulu mkoani kigoma(kulia) akifurahia kwa kupata tuzo ya utendaji bora wa kazi aliyokabidhiwa na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo, Keith Tukei(kushoto) Wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kwa washirika wa kibiashiara na kuwatunuku tuzo na vyeti mbalimbali kwa watendaji bora. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania, Evans Lyimo(kulia) akiongea na baadhi ya washiriki katika warsha ya kutoa elimu kwa washirika wa kibiashiara iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuweza kuendelea kuboresha huduma za kibiashara katika jamii. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mshirika wa kibiashara wa Vodacom Tanzania,Lilian Minja mkazi wa jijini Dar es salaam(kulia) akifurahia kwa kupata cheti cha utendaji bora wa kutoa huduma kwa wateja alichokabidhiwa na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo, Keith Tukei(kushoto) Wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kwa washirika wa kibiashiara na kuwatunuku tuzo na vyeti mbalimbali kwa watendaji bora,katikati ni Andrew Temu. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment