HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 12, 2015

NMB YADHAMIRIA KUINUA WANAWAKE KUPITIA MICHEZO

  Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas (wapili kulia) akimkabidhi jezi Kapteni wa Timu ya Taifa ya Hockey-Wanawake – Kidawa Abdallah (watatu kushoto) leo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo NMB ilitangaza udhamini wake kwa Timu ya Taifa ya Hockey inayotarajiwa kushiriki mashindano ya Afrika kuwania kufuzu mashindano ya Olimpiki (Olympic Qualifier) mashindano yatakayoanza Oktoba 23 mwaka huu. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo – Juliana Soda na Kocha wa Timu ya Taifa ya Hockey – Wanawake – Valentina Quaranta (kulia).
 Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas (wapili kulia) akimkabidhi jezi Kapteni wa Timu ya Taifa ya Hockey-Wanaume – Amarjeet Ruprai.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo – Juliana Yasoda (Wapili kushoto) akikabidhi bendera ya taifa kwa Kapteni wa Timu ya Taifa ya Hockey
Kocha wa Timu ya Taifa ya Hockey – Wanawake – Valentina Quaranta (kulia) akitoa shukurani kwa NMB kwa niaba ya Timu ya Taifa ya Hockey.

NMB YADHAMIRIA KUINUA WANAWAKE KUPITIA MICHEZO
Benki ya NMB imeidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa Hockey katika mashindano ya Africa Olympic Qualifier yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23, 2015 mpaka Novemba 1, 2015 – Johannesburg, Afrika Kusini ikiwa na lengo la kuinua maisha ya wanawake kupitia michezo.

Udhamini huo ni pamoja na kutoa tiketi za ndege kwa wachezaji wote na viongozi pamoja na vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mavazi ya safari kwenda Afrika ya Kusini vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 17.
Afisa wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas alisema benki ya NMB marazote hufarijika inapopata nafasi ya kusaidia michezo kwani kwa kufanya hivyo inaonyesha kujali kwao kwani miongoni mwa wapenda michezo na wachezaji wenyewe, ni wateja wa NMB.

 “Tunaamini michezo ni muhimu katika kubadilisha maisha ya wachezaji ambao wengi wao ni vijana, hivyo udhamini wetu kwa Timu ya Taifa ya mchezo wa Hockey Tanzania utaongeza chachu ya ushindi kwa mchezo ambao unaonekana mgeni Tanzania, tunaamini mchezo huu pia utatoa fursa kwa vijana kupata ajira pamoja na kuitangaza nchi yetu kupitia michezo ya Olimpiki.” Alisema Bwana Barnabas

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad