Nyumba ya familia, inayokaliwa na bibi Siajabu Adam Ali wa kijiji cha Minazini shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba, ambayo ilidaiwa kuchomwa na mdogo wake, Zahara Hamza Adam kutokana na ugomvi wao wa muda mrefu, nyumba hiyo iliteketea kila kitu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
Baadhi ya
vitu vilivokuwemo ndani ya nyumba anayoishi Siajabu Adam Ali, ikiwa ni
pamoja na magodoro, mabegi mawili ya nguo, vitanda, baiskeli na vyombo
vya matumizi ya ndani, vikiwa vimeteketea, baada ya nyumba hiyo kudaiwa
kuchomwa na mmoja wa familia wa nyumba hiyo, Zahara Hamza Adam kwa
ugomvi wa kiamilia na sasa anashilikiwa Polisi.
Siajabu Adam
Ali akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa wa nyumba ya
familia anayoishi, baada ya kuchomwa na mdogo wake Zahara Hamaza Adam,
usiku wa kuamkia juzi, kutokana na hitilafu zao za kifamilia, na
kuiteketeza yote na hakukuwa na mtu aliejieruhiwa.
Sehemu ya ndani ya nyumba ya familia, inayokaliwa na bibi Siajabu Adam Ali na watoto wake wawili, kijiji cha Minazini shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba, ambayo ilidaiwa kuchomwa na mdogo wake Zahara Hamza Adam, kutokana na ugomvi wao wa muda mrefu, nyumba hiyo iliteketea kila kitu.
No comments:
Post a Comment