Mtengenezaji wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia wa Nigeria anayefanya kazi zake nchini Marekani Bi.Florence Ifeoluwa maarufu kama DJ Cuppy akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wa habari wakiwa na Dj Mtengenezaji wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia Nigeria katika hoteli ya Silpway jijini Dar es salaam.
DJ Cuppy.
MTENGENEZAJI wa muziki,
mtunzi wa nyimbo na DJ raia wa Nigeria anayefanya kazi zake nchini Marekani Bi.Florence
Ifeoluwa
maarufu kama DJ
Cuppy amewasili jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Afrika
yenye jina la 'Cuppytakes Africa'.
Wakati akiwa jijini hapa Dj huyu ambaye ni
maarufu sana alitembelea kituo chaKigamboni Community Center kinachotoa elimu
kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Ziara yake ilihitimishwa na
onyesho la muziki lililofanyika katika hoteli ya Slipway,tarehe 16 Agosti,Ziara
yake hii kabambe ya mwezi mzima ilianza Agosti 1 jijini Lagos, Nigeria
ikifuatiwa naSenegal, Ghana na Kenya.
Tanzania ni nchi ya tano katika ziara
yake na hapo DJ Cuppy atatembelea nchi za Rwanda, Uganda na Afrika
Kusini.“Nilikuwa na ndoto ya kutembelea Afrika, lengo kuu likiwa ni kujionea
utamaduni wake, ndotohii sasa imetimia," alielezea katika mkutano na
waandishi wa habari mjini Lagos Julai 8 hukuakiongeza kwamba “nina furaha sana
kuonja radha ya muziki tofauti na kupata uzoefu kutokanana ziara hii!"
Alisema.
Pamoja na hayo, ziara hii inalenga kutoa msukumo katika jamii
kwa kila nchi, DJ huyu mwenyekusherehesha ana shauku juu ya elimu ya
viongozi wa baadaye wa Afrika.
Kupitia msaadamkubwa wa asasi ya Dangote
Foundation, anatembelea na kutoa msaada kwa shirika lisilo lakiserikali katika
kila nchi atakayoitembelea.
Hapa Cuppy ametembelea kituo cha jamii cha Kigamboni kijulikanacho kama (KCC), Kituo hiki huwa kinashughulika na masuala ya kutokomeza umaskini, huku
kikijikita katika kutoa elimu ya chekechea na msingi kwa watoto ambao wako mbali
na upatikanaji waelimu.
KCC pia hutoa fursa nyingine za kujifunza kwa vijana wa
Kigamboni, na pia hutoa elimu ya jamii, madarasa ya kuendeleza vipaji na mafunzo ya ufundi stadi, Ziara hii inayojulikana kwa jina
la “Cuppy takes Africa” wamechagua kituo hiki kwa sababu ya kujitolea kwao
kukuza vipajina kujenga upatikanaji wa elimu kwa jamii.
DJ Cuppy amefanya kazi
katika safu ya tuzo yenye hadhi ya juu ikiwa ni pamoja na FinancialTimes Summit
mwaka 2014 na kwenye tuzo za muziki za MTV Afrika. Yeye ni msomi kutokaChuo cha
London King’s College na sasa anaendelea na masomo ya shahada ya uzamili katika
fani ya Sanaa na biashara ya
muziki kwenye Chuo Kikuu cha New York. Cuppy pia ni balozi wautalii wa
Nigeria.Ziara hii ya “Cuppy takes Africa”' inayojumuisha maonyesho,
mashirikishano ya wasanii, fursaza vyombo vya habari na ushirikiano wa hisani
umedhaminiwa na benki ya GT.
Kuhusu DJ Cuppy:
Cuppy ni DJ, producer wa muziki
na mtunzi wa nyimbo.alizaliwa jijini Lagos mwaka 1992. Cuppy alianza kufanya
uzalishaji wa muziki na baadayekuwa mchezesha muziki (DJ) akiwa na umri wa
miaka 17.Cuppy mara nyingi amekuwa na bahati ya kuwa DJ kwenye umati wa watu
wasomi wakimataifa; alitoa burudani mbele ya wanadiplomasia kwenye mkutano wa
Financial Times Luxury mwaka 2014, ambao ulifanyika jijini Mexico City.
Alikuwa pia DJ katika jarida la Tatlerna Christie Inc Arts Ball, ambao
ulifanyika jijini London ikifuatiwa na matukio mengi yaushirika mjini
Dubai. Kuchaguliawa kwa Cuppy kuwa Dj wakati wa tuzo za muziki za MTV
Afrika mwaka 2014 mjini Durban, ilikuwa ni fahari kwa mashabiki wa Cuppy
duniani kote.
Mwaka jana mwezi Julai
2014, Cuppy ilitoa tepu yake iliyokuwa na mafanikio makubwailiyojulikana kwa jina
la House Of Cuppy. Ikiwa na mkusanyiko wa radha ya muziki tofauti wawasanii wa
kinigeria waliokuwa wanafanya vizuri kimuziki nchini Nigeria. House Of
Cuppyilizinduliwa kwa mafanikio jijini London, Lagos na New York.Cuppy
aliteuliwa na Mheshimiwa Waziri wa Utamaduni na Utalii tarehe 17 Aprili
2014 kuwa Balozi wa utalii nchini Nigeria. Kwa sasa yeye ni nembo ya
kuchochea kampeni ya kuitangaza Nigeria.
“Cuppy ni kijana mjasiriamali,
na ni dhahiri anapaswa kuigwa.

No comments:
Post a Comment