Matope jinsi yalisawazisha eneo la Suna Jangwani jijini Dar es Salaam hadi inashindikana kufunguka kwa baadhi ya milango na mageti. hii ni kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu mizuri ya kupitisha maji katika mto Msimbazi.
Wakazi wa kata ya Suna Jangwani jijini Dar akitoka kwa shida ndani ya nyumba yake ambayo imejaa matope kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha jijini Dar es Salam.
Kijana kama alivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa mtaa katika mtaa wa Suna akisafisha nyumba ambayo imejaa matope kutokana na mvua zilizo sababisha mafuriko maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mzee Mbawala akionyesha jinsi nyumba zilivyo halibiwa kutokana na mafuriko jijini Dar es Salaam katika mtaa wa Suna, tope limejaa mpaka usawa wa dirisha ikiwa mzee huyo alikuwa akinyoosha mkono kabla ya nyumba hii kujaa tope ndipo alipokuwa akigusa dirisha la nyumba hiyo.
Hapa usafi unaendelea katika mtaa wa suna Jangwani jijini Dar es Salaam.
Huyu mama kaona ajihifadhi katika kibanda kilichopo pembeni ya nyumba yake ili kupisha usafi wa kutoa tope ndani ya nyumba yake.
Hili ni Jengo mojawapo la Hospitali ya Mhimbili linalopakana na mto Msimbazi jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment