HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 12, 2015

BARCELONA VETERANS NA TANZANIA VETERANS WALIVYOKIPIGA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

Wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania wakiongozwa na Patrick Kluivert (aliebeba mtoto) wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Tanzania Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. hadi mwisho wa mchezo, Barcelona ya Hispania ilishinda bao 2-1.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert akifurahia jambo na Mtoto mwenye Ualbino kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo, pia kulikuwa na ujumbe wa Harakati ya Imtosha ikiwa ni kupiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino nchini.
Mshambuliaji Machacha wa Liverpool na Barcelona enzi hizo, Luis Garcia akionyesha ufundi wake mbele ya wachezaji wa Tanzania Veterans, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliopogwa kwenye uwanja Taifa, Jijini Dar es salaam.
Beki wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa "Fusso" akimzungusha mshambuliaji wa Barcelona Veterans.
Nyanda wa Tanzania Veterans, Peter Manyika akiruka kuondosha hataro langoni mwake.



















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad