HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 24, 2015

KAMERA YA MTAA KWA MTAA NA TASWIRA MBALI MBALI KUTOKA MAHAKAMA YA NDIZI,MABIBO JIJINI DAR

Kamera ya Mtaa kwa Mtaa Blog,leo hii ilipata wasaa wa kukatiza kwenye Soko la Ndizi Mabibo (maarufu kama Mahakama ya ndizi) jijini Dar es salaam na kufanikiwa kunasa taswira mbalimbali katika soko hilo maarufu hapa jijini Dar.Soka hili linasifika sana kwa kuwa na ndizi za kila aina nyingi na zinazotoka katika mikoa ya Mbeya,Kilimanjaro na Kagera.Pichani ni mmoja wa wauzaji wa ndizi hizo akiwa amebeba mkungu kuutoa sehemu moja kwenda nyingine.
Ndizi aina ya Mshale zilisubiri kushushwa kutoka kwenye lori lililokuwepo sokoni hapo.
Wafanyabiashara wa soko hili,muda wote wako bize,kwani wateja hawakatiki sokoni hapo hasa siku za mapumziko ya wiki kama leo.
Ndizi zikipakiwa kwenye Mkokoteni.
Mandhali tulivu ya soko hilo kama ilivyonaswa na Kamera ya Mtaa kwa Mtaa leo.
Mzee wa kubeba dabo dabo akiwahisha ndizi kwa mteja.
"......hizi zote bei gani?...." Wanaonekana Wateja hao wakimuuliza muuzaji.
Hizi nazo zimevundikwa kwa utaalamu wa kuzivunika kwa majani ya mgomba.
Maparachichi nayo yanapatikana kwenye shoko hili la Mahakama ya ndizi.
Mapasheni pia ndani.
Mananasi ndio usiseme,maana ni kama uzao wake unaendana na ndizi hizo.
Viazi ulaya.
Mzigo mwingine ukiendelea kushuka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad