HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 5, 2014

TAARIFA - TUME YA UCHUNGUZI OPERESHENI TOKOMEZA YAANZA RASMI KUPOKEA TAARIFA NA MALALAMIKO

Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza ujangili inatoa taarifa kwa umma kuwa imeanza rasmi kupokea taarifa na malalamiko mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili nchini.

Katika kufanikisha majukumu yake, Tume itatembelea maeneo mbalimbali nchini ili kukutana na wananchi wenye tarifa au malalamiko kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

Aidha, Tume inawaarifu wananchi kuwa taarifa au malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni hiyo yatapokelewa kwa njia ya posta, barua pepe na simu za mkononi kama ifuatavyo;
i.                    Katibu wa Tume,
Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili,
SLP 9050,
Kivukoni Front,
Dar es Salaam

ii.                  Barua pepe: opereshenitokomeza@agctz.go.tz
iii.                Namba za simu
Tigo:                0714 826826
Vodacom:       0767 826826
Airtel:              0787 826826
Zantel:             0773 826826

Imetolewa na:
(signed)
Fredrick K. Manyanda
KATIBU WA TUME

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad