Katika maendeleo ya jamii yoyote, moja ya kitu muhimu ni kukuwa kwa maarifa ya wanajamii. Maarifa yatakayowapa uwezo wa kutumia ujuzi kwenye kutenda. Haijalishi upo kwenye fani gani, bali siku ya mwisho ni lazima uweze kutenda na siyo kuishia vitabuni.
Kwa miaka mingi, nimekuwa nikifuatilia tatizo la ajira, umasikini nk hapa nchini, ingawa kuna mambo mengi sana ndani yake, lakini mzizi wa yote ni maarifa. Kizazi chetu SIYO kizazi cha watu wenye maarifa. Hii inawezekana ni kutokana na uvivu wa kujifunza au kutokuwa na nyenzo za kujifunza. Na kwakuwa na kizazi cha watu wasio na maarifa, kinapelekea kurudisha nyuma mambo mengi sana.
Leo hii, kazi nyingi zinafanywa nje ya nchi, hata Toothpick tunaagiza kutoka nje, leo hii ukienda Supermarket zaidi ya asilimia tisini ya vitu, vinatoka nje. Sasa, swali la kujiuliza je hapa nyumbani hatuna watu wenye uwezo wa kutenda? Jibu, ni tunao, ila ni wachache na kasumba yetu inatuumiza pia wengi hawajiamini.
Kitu ambacho nimejifunza na kukipenda nilipokuwa China (kwa miaka tisa) ni jinsi gani Wachina wamefanikiwa kujenga kikazi chenye maarifa. Na wana njia nyingi sanasana za kujifunza na siyo lazima uende chuoni.
Na wameweza kuitumia lugha yao kuwawezesha watu wake, Jiulize, leo hii hapa nyumbani kuna sehemu ngapi za kujifunza bila kulipia gharama ya ziada? Jiulize, leo hii kama utapata tatizo la kiufundi, kuna mtandao gani unaweza kutuma tatizo lako na ukapata msaada wa haraka? Ni michache sana sana kama siyo hakuna.
Hivyo basi, katika kuhakikisha wanajamii wa Kitanzania wanapata maarifa, wale walio vyuoni wanajifunza kwa ufanisi (hawatoki wakiwa wamekariri tu), na wale walio mitaani wanajinoa na kuhakikisha wanakuwa wapya kila siku.
Tunakuletea Dudumizi Forums , uwanja wa kujinoa maarifa ya IT. Ni uwanja utakaoweza kusoma, kuuliza na kijiendeleza zaidi. Ni uwanja huru kwa wanajamii wote wenye moyo na hamu ya kujifunza na kusaidiana kwenye IT ili kufikia malengo. Jumuika sasa.
Tembelea Dudumizi Forums forum.dudumizi.com
Huu ni mwanzo tu, katika kuhakikisha tunajenga jamii yenye maarifa, mambo mengi yatawajia toka Dudumizi kadri siku zinavyozidi kusonga . Hivyo, kuwa pamoja nasi.
No comments:
Post a Comment