Nyomi ya wati imetapakaa katika eneo la shopping mall ya Mlimani City jijini Dar es salaam muda huu baada ya Super Market mpya ya NAKUMATT HOLDINGS iliyoinunua Shoprite STORES kufanya SELI ya 50% kwa bidhaa zote zilizokuwepo kwenye Super Market hiyo, ili kupisha mzigo mpya. Pichani ni baadhi ya watu wakichangamkia SELI ya bidhaa hizo.
Hili ni Nyomi linaloonekana kwa nje na ndani kuna idadi kuwa ya watu waliobahatika kuingia toka asubuhi,kwa ajili ya saula saula hiyo ya bidhaa. Milango ilifungwa kutokana na kutokea kwa vurugu kubwa la watu waliojitokeza kwa wingi kwenye Super Market hiyo.
Wengine wameamua kukaa chini kusubiri bahati ya kuingia ndani ya Super Market hiyo kujipatia chochote kwa bei chee.
No comments:
Post a Comment