HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 24, 2014

MPANGO MZIMA WA USAFI WA JIJI WAIPENDEZESHA KARIAKOO JIJINI DAR

 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa imebahatika kukatiza mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaama na kuijionea hali na spidi nzuri ya kulitembeza fagio kisawasawa eneo hilo la Kariakoo na kuridhishwa na hali hivyo.ndugu Mdau hutakiwa kuandikia mate na wakati wino upo,hebu tupia macho yako kwenye taswira mbali mbali na za kupendeza kabisa ndani ya eneo hilo.Picha na Mwanalibeneke Philemon wa Mtaa kwa Mtaa Blog.
 Kichuguu cha kiaina kikiwa na tangazo la kupendeza kabisa.
 Mambo ni swadakta kabisa kama unavyoona mwenyewe.Pongezi nyingi kwa Manispaa ya Ilala kwa kazi nzuri wanayotuonyesha wananchi wao.
 Kutokana na sehemu kubwa ya eneo la Kariakoo kuwa safi kupindukia,hali inayopelekea hata vijana wa maeneo hayo kuonyesha michezo yao kuu ya utelezi kama hivi.
 Ukikaa kariakoo wala huna haya ya kwenda Bichi,wee toka tu nje na kiti chako na maji utanaona na hata ukitaka kuogelea pia inawezekana kabisa.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad