baadhi ya mabasi yaendayo mtwara yakiwa mjini Lindi toka jana baada ya mgomo huo kuhofia usalama.
Askari Polisi wakiwa tayari kwa ulinzi na kuyasindikiza mabasi hayo mpaka mkoani Mtwara.
Mmoja wa Madereva wa Mabasi akiongea na waandishi wa habari.
Badhi ya Abiria wakiwa kituo cha mabasi mjini Lindi bila kuelewa hatma ya safari yao hii leo.
KAMANDA wa Polisi mkoa wa Lindi George Mwakajinga akiwasihi madereva kuridhia kusindikizwa na polisi kwenda mtwara.
Na Abdulaziz Video,Lindi
Zaidi ya Abiria 400 Waliokuwa wanafanya safari kati ya Dar es salaam na Mtwara jana wamelazimika kusitishiwa safari mkoani Lindi kufuatia madereva na wamiliki wa Mabasi waliyokuwa wanasafiria kuogopa kutokana na hali ya Amani kutokuwepo Mkoani Mtwara kufuatia Vurugu za Mgogoro wa Gesi.
Ripota wetu alifika katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Lindi na kukuta msongamano Huo ambapo Jeshi la Polisi Mkoani Lindi likiongozwa na kamanda wa Polisi wa Mkoa,George Mwakajinga Likitoa ulinzi kwa mabasi hayo kuyafikisha Mtwara hali ambayo imekataliwa na Madereva wa Mabasi pamoja na baadhi ya Abiria.
Kamanda Mwakajinga akiongea na blog hii alieleza kuwa sambamba na kuhakikishiwa Usalama wa mabasi hayo kwenda Mtwara alishangazwa na baadhi ya madereva kugoma kusindikizwa na Polisi kwa hofu ya Usalama wa Magari na Abiria wanaowasafirisha.
Mwandishi hakika Jeshi limejipanga kuwasindikiza hadi mtwara ila nimepigwa na butwaa baada ya abiria na Madereva kugoma kwenda mpaka sasa sijui tufanye nini maana sasa ni mgomo huu ila nakuhakikishia bado tutawapa Ulinzi wa Kutosha na watakuwa salama.
Baadhi ya Madereva wa Mabasi hayo walieleza hofu yao kuhusu kuendelea na safari huku baadhi ya Abiria wakiwa na misimamo Tofauti kuhusiana na Hali hiyo Ambapo wengine wanalazimishwa kusafiri wengine wakihofia usalama wao huku madereva wakikataa kuondoka Lindi.
Asubuhi Mmiliki wa Basi la Buti la Zungu,Zubeiry Namachokole ameamua kutoa gari yake nyingine aina ya Coaster kuwapeleka abiria wake waliolala Lindi badala ya Basi yake ya Yutong kuhofia usalama wa Basi hilo.
Hadi tunakwenda Mitamboni abiria wengi walikuwa wakihangaika kwa makondakta na Madereva huku wakitafuta msaada wa Serikali ili wasaidiwe chakula na hifadhi hadi hali itakaporejea kuanza safari kutokana na wengi kusafiri wakiwa na hali ngumu wakiwemo akina mama na watoto
No comments:
Post a Comment