Mzee wa Mtaa kwa Mtaa habari za leo.
Kutokana na mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha hapa Dar es salaam, sehemu hii ya barabara ya Mwepu kando kabisa ya jengo la Wizara ya Katiba na Sheria imeharibika kwa kutitia na kutengeneza shimo ambalo sio tu linahatarisha maisha ya watumiaji wa barabara hiyo lakini linaleta usumbufu na foleni kubwa. Ni takribani wiki zaid ya mbili sasa lakini wahusika hawajachukua hatua yoyote. Tunaomba wahusika wachukue hatua ili kulinda usalama wa watumiaji wa barabara hiyo muhimu.
Zifuatazo ni picha zinazojieleza zenyewe kusaidia wahusika kuona hali halisi.
Shukrani kaka
No comments:
Post a Comment