HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 15, 2013

PPF YAENDELEA KUANDIKISHA WANACHAMA WAPYA KATIKA WIKI YA HIFADHI YA JAMII

Mbungewa Jimbo la Tabora Mjini Mh. Aden Rage akikabidhi mchango wake wa kwanza kwa Mhasibu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Grace Fihavango mara baada ya kujiunga na Mfuko huo. Mheshimiwa Rage alijiunga na PPF chini ya mfumo wa hiari alipotembelea banda la PPF kwenye wiki ya Hifadhi ya Jamii inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw. William Erio.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw. William Erio (kushoto) akimkabidhi kitambulisho cha uanachama wa PPF Mbunge waTabora Mjini Mh. Aden Rage (katikati) mara baada ya kujiunga na Mfuko huo. Mheshimiwa Rage alijiunga na PPF chini ya mfumo wa hiari alipotembelea banda la PPF kwenye wiki ya Hifadhi ya Jamii inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Eliudi Sanga.
 MbungewaJimbo la TemekeMh. Abbas  Mtemvu akipata maelezo ya fomu ya kujiandikishana Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka kwa Afisa Michango wa PPF Bi. Herieth Magala. Mhe.Mtemvu aliamua kujiunga na PPF alipotembelea kwenye banda hilo, katika wiki ya Hifadhi ya Jamii inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.

Mbungewa Jimbo la TemekeMh. Abbas Mtemvu akikabidhi mchango wake wa kwanza kwa Mhasibu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Grace Fihavangomara baada ya kujiunga naMfuko huo. Mheshimiwa Mtemvu alijiunga na PPF chini ya mfumo wa hiari alipotembelea banda la PPF kwenye wiki ya Hifadhi yaJamii ya inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.  Katikati ni Afisa Michango wa Mfuko huo Bi. Herieth Magala akishuhudia tukio hilo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad