Mwenyekiti mpya wa bodi ya chuo cha mahusiano ya kimataifa na diplomasia mh balozi mwanaidi maajar akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo inayoundwa na wajumbe tisa waliobobea katika fani ya utatuzi wa migogoro na Diplomasia.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh Benard Membe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Chuo cha Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.Bodi hiyo inaundwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya mahusiano ya kimataifa na diplomasia wapatao tisa chini ya uenyekiti wa Mh balozi Mwanaidi Maajar Mh Membe ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inafanya kazi ya ziada ili chuo kiwe na uwezo wa kijiendesha chenyewe ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kinazidi kujiimarisha zaidi katika utoaji wa kozi za utatuzi wa migogoro, Lakini pia amekitaka chuo hicho kuhakikisha kinatafuta chuo washirika nje ya nchi ilikubadilishana uzoezi ikiwa ni pamoja na kuwa na program ya kubadilishana wanafunzi.
Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh John Haule akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mh Benard Membe kwa ajili ya uzinduzi rasm wa bodi mpya ya Chuo cha Mahusiano ya kimataifa na Diplomasia, hafla iliyofanyika chuni hapo.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikino wa kimataifa Mh benard membe akiteta jambo na mwenyekiti mpya wa bodi ya chuo cha diplomasia na mahusiano ya kimataifa mh balozimwanaidi maajar |katikati} kulia ni mkurugenzi wa chuo cha diplomasia na mahusian ya kimataifa mh balozi dk Mohamed maundi.
Wajumbe wa bodi ya chuo cha mahusiano ya kimataifa na diplomasia wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa mambo ya nnje na ushirikiano wa kimataifa mh benard membe muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa bodi hiyo, Bodi hiyo mpya iko chini ya uenyekiti wa Mh Balozi Mwanaid Maajar, ambapo wajumbe ni pamoja na Balozi Abdi Mshangama, Dr. Leonidas Mushokolwa, Mh. Saidi Mtanda MB, Mh. Betty Machangu MB, Mr. Affan Maalim,Mr. Dushhood Mndeme, Mr. Harold Utouh na Mr .Abdulrahman Abdallah.
No comments:
Post a Comment