Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kanali Joseph Simbakalia akifungua Warsha ya Majadiliano ya Ushirikiano wa Kibiashara kwa Manufaa ya Umma Kikanda kwa Wawakilishi toka Mikoa ya Lindi,Ruvuma na Wenyeji Mtwara,Kulia ni Samson Chemponda,Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara na kushoto ni Saidi Masudi Nahunda,Mwenyekiti wa TCCIA-Mtwara.
Wadau mbalimbali wanaohudhuria kikao cha mashirikiano ya kibiashara kutoka mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma kinachoendelea katika Ukumbi wa Makonde Beach Resort-Mtwara.
Na Abdulaziz Video-Mtwara
Wadau
mbalimbali wa Serikali,Wafanyabiashara na wanahabari toka Mikoa ya
Lindi,Mtwara na Ruvuma wanakutana leo katika warsha ya mashirikiano ya
kibiashara kwa mikoa hiyo wanakutana leo ili kujenga na kubadilishana
mawazo kwa lengo la kujenga uelewano na Ushirikiano ambao utasaidia
kutekeleza Dira ya kibiashara kwa Ufanisi.
Majadiliano
hayo ya ushirikiano yatachangia katika kusukuma mbele utekelezaji wa
Dira ya Tanzania ya Maendeleo 2025 pamoja na juhudi mbalimbali kuendelea
utekelezaji wa Dira hiyo hauendani na shabaha ya kuiwezesha nchi ya
kipato cha kati inayojivunia maendeleo makubwa na maisha bora ya
wananchi.
Katika
warsha hii mada kuu ni kuhamasisha Teknolojia kwa mageuzi ya kiuchumi
na kijamii Tanzania itawasilishwa ikienda sambamba na mada ndogondogo
ikiwemo Umuhimu wa Ubunifu katika mageuzi ya kiuchumi na kijamii,Mchango
wa Tehama,Ubora wa Viwango katika wilaya,usalama wa watu na mali zao
ikiwa pamoja na majadiliano ya Vikundi mada ambazo zitatolewa na
UDSM,COSTECH,TCRA,TBS na Polisi Makao Makuu
No comments:
Post a Comment