FOWARD MOTION ikishirikiana na Dorctor's Plaza Heart Clinic pamoja na Lancet Laboratories wamezindua mpango wa upimaji afya (Medical checkup) mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Doctor's Plaza Heart Clinic yaliyopo Sea View jijini Dar es salaam.
Katika siku hii washirika hao walitoa huduma ya bure ya upimaji wa Cholestrol, Sugar, Blood Pressure, ECG na BMI. Waalikwa wote walipata fursa ya kupima vipimo hivyo na kupata ushauri wa bure (free consultation) kutoka kwa madaktari Bingwa Campaign hiyo pia iliambnatana na mafunzo mbalimbali ya afya kutoka kwa mabingwa hao.
Kwa mujibu wa msemaji wa DPHC, Bi Sofia Byanaku, Mpango huo endelevu, utaendelezwa kwa njia tofauti na ngazi tofauti, akisisitiza kuwa Kinga ni bora kuliko Tiba!
Wadau wakisikiliza maelezo toka kwa madaktari kuhusu umuhimu wa kupima afya
Dkt Masatu akitoa elimu ya bure kuhusu umuhimu wa watu kupima afya zao
Dkt Vivian mlawi akitoa ushauri kwa Nancy Sumary aliyekuwa mmoja wa wadau waliofika kupata huduma hiyo ya bure ya kupimwa afya na kupewa ushauri
wadau wakisubiri zamu kupimwa
Nesi akimpima bloga maarufu Missie Popular
Doctor's Plaza Heart Clinic ilihudumia wadau kibao siku hii
Wafanyakazi wa Doctor's Plaza Heart Clinic wakijadiliana namna ya kuendesha kazi siku hii
Mama akijiandikisha Doctor's Plaza Heart Clinic
Kumbukumbu zinawekwa kwa uangalifu
No comments:
Post a Comment