HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 30, 2013

Mbeya kuingia Digitali leo

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema mitambo ya Analojia mkoani Mbeya itazimwa rasmi leo saa 6:00 usiku. 

Akizungumza na waandishi habari, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, alisema Mkoa wa Mbeya umekuwa wa mwisho katika hatua za kuzima mitambo hiyo, katika awamu ya kwanza. 

Mungi alisema uzimaji wa mitambo ya analojia na kuhamia katika mitambo ya Digitali katika awamu ya kwanza, ulihusisha Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Mwanza, Moshi na Arusha. 

Alisema wakazi wa Mbeya walikwishafahamishwa kuhusu kuzimwa kwa mitambo hiyo kwa kufanya maandalizi yaliayohitajika ili kuepuka usumbufu ambao ungejitokeza. 

Aliwataka Watanzania kuacha kunung’unika wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali na hasa yanayohusu matatizo ya ving’amuzi na badala yake, wachukue za kutafuta ufumbuzi Alisema baadhi ya Watanzania wamekuwa wakitumia muda mrefu kunung’unika na kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad