Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo kasi,unaendelea katika Barabara ya Morogoro rodi na hapa ni katika Daraja la Manzese jijini Dar ambapo sehemu ya nguzo zake zimipitiwa na greda ili kuweka sawa Barabara hiyo mpya ambayo kwa spidi ya ujenzi inavyoendelea huenda ikamalizika mapema sana mwakani.Redio mbao zinasema kuwa Mabasi hayo ya kasi yatakuwa yakipita katikati ya barabara za pande zote mbili,sasa sijui ndio maana wameamua kupitisha greda katika nguzo za daraja hili??
Makaravati yaliyokuwa yamewekwa mitaroni yakiwa yamekula sururu na kuwekwa kando ili kupisha ujenzi wa Barabara hiyo.



No comments:
Post a Comment