Dhana ya kwamba shule zote za kata ziko katika mazingira magumu na hazifanyi vema katika maendeleo ya elimu hapa nchini si sahihi kwani kuna baadhi ya shule za sekondari za kata ambazo zina maendeleo mazuri sana kitaaluma kushinda hata zile shule kongwe za serikali na shule nyingi za binafsi. Fuatana na mwandishi wetu Abraham Lazaro wa Shirika la HakiElimu aliyefanya ziara hivi karibuni katika wilaya ya Arusha na kuitembelea shule ya kata ya Kaloleni.Pichani ni Shule ya Kaloleni Mjini Arusha iliyoanzishwa mwaka 1998, ilishika nafasi ya 12 kati ya shule zote 137 zilizofanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2011 katika mkoa wa Arusha.
Motto wa Shule “ Matunda ya elimu huwa ni matamu lakini.......” Nidhamu ni kitu ambacho kinazingatiwa na uongozi wa Mwalimu Munga ,usiombe ukutwe na makosa , hii ni siri kubwa ya mafanikio waliyonayo shule ya Kaloleni.
Jengo la utawala na ilipo maktaba ya shule ya kata ya Kaloleni lilojengwa kwa ufadhili wa JICA.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Mrs Machange M.J akifanya mahojiano na mwandishi.
Sayansi bila vitendo haiwezekani, shule hii ina maabara za masomo yote matatu ya bailojia, fizikia na kemia.
Sehemu ya maegesho ya magari ya wafanyakazi na wageni katika shule ya kata ya kaloleni.
Maelezo ya sehemu mbalimbali zinazopatikana katika shule hii.

No comments:
Post a Comment