HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 14, 2012

Japhet Kaseba na Francis Cheka kuzichapa Julai 7

Mabondia, Francis Cheka (kushoto) na Japhert Kaseba, wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Siku ya tarehe saba mwezi wa saba katika uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salaam.

Katika Mpambano huo ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii muziki wa bongo fleva nchini wakiongozwa na Diamond pia kutakua na mechi ya Bongo Movie na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano uho ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na Kaike Siraju na utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa

Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni Adiphoce Mchumiatumbo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashidi Ali huku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na Said Mbelwa wakati bondia chipukizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D' watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad