Msemaji wa Klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga(kushoto)akisalimiana na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa wakati walipofika katika viwanja vya TCC kuuaga mwili wa aliekuwa mchezaji wa klabu hiyo marehemu Patrick Mafisango na kutoa mkono wa pole wa kiasi cha shilingili 1M/-kulia ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akimkabidhi rambirambi ya kiasi cha shilingi 1M/-mjumbe wa kamati ya utendaji na Makamu mwenyekiti wa kamati ya fedha wa klabu ya Simba Bw.Saidi Pamba,anaeshuhudia katikati ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa pamoja na Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania,Ibrahim Kaude wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliekuwa mchezaji wa klabu ya Simba,marehemu Patrick Mafisango kwenye Viwanja vya TCC,Chang'ombe jijini Dar.
No comments:
Post a Comment