Mchezaji wa Timu ya Chuo cha KCMUCO upande wa wanawake, Suche Atanasia akionyesha umahiri wake wa kuchenza Pool katika mashindano ya Pool Higher Learning Mkoa wa Kilimanjaro.
Mchezaji wa Timu ya Chuo cha MUCCOBS upande wa wanawake,Maryvianney Chizziel akionyesha umahiri wake wa kuchenza Pool katika mashindano ya Pool Higher Learning Mkoa wa Kilimanjaro.
Wachezaji wa Chuo cha MUCCOBS wakishangilia mara baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano hayo.
Ofisa mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro, Edmundi Rutaraka (wapili kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya mchezo wa Pool ya Chuo cha MUCCOBS zawadi ya ushindi wa kwanza Shilingi laki tano.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Kilimanjaro, Christopher Shitungu.
Nahodha wa chuo cha SMMUCOBS akionyesha zawadi yao ya Shilingi laki tatu (300,000/=) baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo.
Mshindi wa Singles wanawake, Suche Atanasia kutoka chuo cha KCMUCO akicheza.
Wachezaji wa Chuo cha MUCCOBS wakipokea kitita cha Shilingi laki tano (500,000/=) mara baada ya kuibuka washindi wakati wa mashindano ya Pool Higher Learning yaliyomalizika mwishonimwa wiki Mkoani Kilimanjaro.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Kilimanjaro, Christopher Shitungu na wa pili kulia ni Ofisa mauzo wa Mkoa wa Kilimanjaro, Edmundi Rutaraka.
MASHINDANO ya Pool Higher Learning Mkoa wa Kilimanjaro Chuo cha MUCCOBS wameibuka mabingwa wa mchezo huo katika Mkoa wa Kilimanjaro hivyo kujinyakulia kitita cha Shilingi 500,000/= baada ya kuwafunga chuo cha SMMUCO pointi 14-11wakati wa chezo wa fainali ulichezwa katika Klabu ya Makanyaga Kata ya Soweto Manispaa ya Moshi Mjini.
Washindi wa Pili katika Mashindani hayo ni SMMUCO ambao walizawadiwa kitita cha Shilingi 300,000/=,washindi wa tatu ni KCMUCO walipata 200,000/= na wane ni chuo cha MWUCE ambacho kilizawadiwa Shilingi 100,000/=
Upande wa Single wanaume(mmoja mmoja), Alphael kutoka chuo cha MWUCE alitwaa ubingwa na kujitwalia 150,000/=akifuatiwa na Beatus Pius kutoka chuo cha MUCCOBS ambaye alishika nafasi ya pili na kujitwalia 100,000/= na Upande wa Singles wakinadada, Suche kutoka chuo cha MWUCE alitwaa ubingwa na kuzawadiwa 100,000/= na kufuatiwa na Maryviana kutoka Chuo cha MUCCOBS na kuzawadiwa 50,000/=
No comments:
Post a Comment