HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 11, 2012

KOCHA MPYA WA TAIFA STARS TANGAZWA LEO JIJINI DAR

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Leodigar Tenga (katikati) akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar es Salaam leo wakati wa Mkutano wa kumtambulisha kocha mpya wa Timu ya Taifa (Taifa Stars).Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ni Wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa,George Kavishe  na Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Angetile Osiah.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ni Wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),George Kavishe (katikati) akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Leodigar Tenga na Kulia ni Kocha Mpya wa Timu hiyo ya Taifa,Kim Poulsen.
Kocha Mpya wa Timu ya Taifa,Kim Poulsen akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa Kocha Mpya wa kuifundisha Timu ya Taifa leo.

Kim Poulsen ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) kuanzia Mei 11 mwaka huu kuziba nafasi ya Jan Poulsen.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema Kim amepewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Shirikisho kuamua kutomuongezea mkataba Jan. Mkataba wa Jan uliokuwa wa miaka miwili unamalizika Julai 30 mwaka huu.

Amesema kwa vile Taifa Stars inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Dunia raundi ya pili Kanda ya Afrika na mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN), TFF imeona ni lazima iwe na kocha mpya mapema kabla ya mkataba wa Jan kumalizika.

Kim ambaye ni raia wa Denmark amekuwa nchini kwa mwaka mmoja sasa akifundisha timu za Taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na miaka 20 (Ngorongoro Heroes), hivyo anawafahamu vizuri wa wachezaji wa Tanzania.

TFF imeanza mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa timu za vijana atakayeziba nafasi ya Kim. Ili kuwa na makocha wenye falsafa moja, kocha huyo anatafutwa kutoka Denmark.

Naye Kim ambaye Jumatatu (Mei 14 mwaka huu) atatangaza kikosi cha Taifa Stars ambacho Juni 2 mwaka huu kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mashindano amesema yuko tayari kwa kazi hiyo na kusisitiza kuwepo ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali ili timu hiyo iweze kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad