HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 13, 2012

KIKULA SPORTS DAY BONANZA

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula alipokua akifungua bonanza hilo ambapo ilikua ni siku ya mwisho ya fainali ambapo karibia michezo yote ilikua ikikutana kwenye fainali.
Timu za Mpira wa Miguu Kutoka Vitivo Vya Sayansi ya Jamii na Kutoka Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa mbele ya jukwaa la mgeni rasmi Prof Idris Kikula Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)(Hayupo Pichani).Kutoka Kushoto Wenye Jezi za Blue Ni Timu kutoka Kitivo Cha Elimu na Mwenye Jezi za Orange ni timu ya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii Zote Kutoka UDOM

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula Kisalimiana Na Wachezaji Wa Timu ya Mpira wa MIguu kutoka Kitivo Cha sayansi Ya Jamii kabla ya Mchezo wao Wa Fainali na Timu ya Kitivo Cha Elimu
Mchezaji wa Timu ya Kitivo Cha Elimu Edward Mzelu alipopiga Penati ya Mwisho Na Kuipa Ushindi wa Magoli 5 kwa 4 dhidi ya Timu ya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii na Kitivo Cha elimu Kuibuka Washindi wa Mashindano ya Kikula Sports Day Bonanza
Mashabiki pamoja na wachezaji wa kitivo cha elimu wakishangilia mara baada ya kuibuka washindi kwa kuifunga kitivo cha sayansi ya jamii kwa mikwaju ya oenati 5 kwa 4
Mchezo wa Netball Kati ya Kitivo Cha Elimu Na Kitivo cha Sanaa na Lugha ukiendelea na Kitivo Cha  Elimu kuibuka washindi.
  Mechi kati ya Kitivo cha Elimu na Kitivo cha Sayansi ya Jamii ukiendelea na Kitio cha sayansi ya jamii kiibuka mshindi katika mechi hiyo.
Washiriki wa Shindano la Kula Hao wakiendelea kushindana Kula katika Bonanza la Kikula Sports Day lililofanyika Jana katika Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma.
Prof Idris Kikula (Katikati) akitabasamu wakati mchezo wa kukimbiza kuku kwa wafanyakazi ukiendelea katika bonanza lililofanyika jana Katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Meneja Wa Kampuni Ya Coca Cola Kanda ya Kati Dodoma Bwana Maginga Akitoa Shukrani ka Uongozi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Na Vilevile Ndio KAmpuni iliyodhamini bonanza hilo Na Hapo alikua akikabidhi Zawadi Za Kreti za Soda kwa Uongozi Wa Chuo Kwaajili ya Kukabidhi kwa Washindi Wa Michezo Mbalimbali
Msanii Chipukizi Chipoka akitoa burudani katika bonanza hilo lililofanyika jana katika Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Tukibadilishana Mawazo na Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)Prof Idris Kikula (Wa pili Kulia), Wa Kwanza Kulia Ni Mmiliki na Mwandaaji Wa Mtandao Huu Wa Lukaza Blogu Bwana Josephat Lukaza, Wa Kwanza Kushoto Ni Kijana Abdul na Wa pili Kushoto Ni Mkuu wa Masomo ya Shahada ya Kwanza Prof Msofe tulipokutana Jana Katika Bonanza La Kikula Sports Day

Baadhi ya Wanafunzi Waliojitokeza Kutazama na Kushuhudia Bonanza Hilo lililofanyika Jana KAtika Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambapo bonanza hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Coca Cola pamoja na Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula.Picha Zote Kwa Hisani ya Josephat Lukaza wa http://josephatlukaza.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad