Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Edward Lowassa (kulia) akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Nchi ya Morocco,Mh. Mohamed Yatim (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao na Spika wa Bunge la Morocco..
Wajumbe wa Kamati ya Bunge la Tanzania ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Edward Lowasa (wa tano kushoto) wakikaribishwa kwenye Kikao na Spika wa Bunge la Seneti la Nchi ya Morocco,Mheshimiwa Mohamed Yatim (kulia).
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Edward Lowassa (wa nne kulia) na Makamu wake,Mh. Mussa Zungu (wa tatu kulia) katika kikao cha pamoja na Makamu wa Rais wa Bunge la Wawakilishi la Nchi ya Morocco. Kamati hii ipo ziarani nchini Morocco.
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Edward Lowassa wakiwa kwenye kikao na baadhi ya Wenyeviti wa Kamati za Bunge la Wawakilishi wa Nchi ya Morocco.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Seneti la Nchi ya Morocco,Mh. Mohamed Yatim.
No comments:
Post a Comment