HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 13, 2012

‘Castle Lager Superfans’ kuzinduliwa rasmi leo Mbalamwezi Beach Jijini Dar

Na Mwandishi Wetu

MASHABIKI wa Ligi Kuu ya England mbayo msimu huu inafunguliwa leo, wanapata bahati tena ya kufurahia soka hilo, baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Castle Lager,kuzindua kampeni ya kupata shabiki bora itakayojulikana kama ‘Castle Lager Superfans’.

Kampeni hiyo inazinduliwa leo katika ufukwe wa Mbalamwezi uliopo Mikocheni, Dar es Salaam ambapo pia kutakuwa na mechi kadhaa za mashabiki wa timu mbalimbali za England, wataokuwa wakifurahia kufungwa kwa msimu wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo amesema kampeni hiyo ni mahususi kwa ajili ya kupata shabiki bora wa Ligi Kuu ya England hapa nchini.

Kabula alisema, shabiki huyo ataungana na mashabiki wengine watano kutoka nchi nyingine za Afrika ambao wataunda kikosi cha ushangiliaji kitakachojulikana kama Africa United, ambacho kitahudhuria fainali za Kombe la Mataifa Afrika zinazotarajiwa kufanyika Afrika Kusini mwakani.

“Kama ambavyo wapenzi wa bia ya Castle Lager na mashabiki wa Ligi Kuu ya England wanavyofahamu, bia yao ya Castle Lager imekuwa mstari wa mbele kuwasogeza karibu na mechi kali zaidi duniani kutoka katika ligi bora kwa sasa, tumeamua kufunga msimu kwa bonanza maalumu na kuufungua kwa kusaka shabiki bora.

“Kwa sasa tunafunga msimu wa Ligi Kuu ya England, huku tukifungua kampeni hii ya kumsaka shabiki bora na aliyebobea katika ligi hiyo. Tutakuwa na utaratibu ufuatao; kampeni hii itaendeshwa nchi nzima na tutapata mashabiki sita, ambao wataingia katika hatua ya kupigiwa kura kwa utaratibu utakaotangazwa baadae,” alisema.

Mshindi wa Castle Lager Superfan 2012 ndiye atakayepata nafasi ya kuhudhuria fainali hizo, huku akilipiwa gharama zote zinazohusu safari, ikiwa pamoja na malazi na chakula kwa kipindi chote atakachokuwa huko.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad