HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 9, 2012

Basi la Muro Investment lawaka moto Mkoani Morogoro

Basi la abiria la Kampuni ya  Muro Investment, lenye nambari za usajiri T 820 BEY lillilokuwa likitokea Jijini Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku jana, haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo. Basi hili ni la pili kwa kuteketea kwa moto ndani ya wiki hii baada ya Basi la Sumry kuteketea kwa moto  Mkoani Dodoma.Picha na Father Kidevu Blog.
 Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.
Wakazi wa Maseyu na wasafiri wakiangalia basi hilo likiteketea kwa moto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad