HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 9, 2012

Airtel yawatangaza washindi bora 10 wa Promosheni ya “Nani Mkali”

Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitangaza majina10 ya washindi 10 bora wa promosheni ya ‘Nani Mkali’ inayoendeshwa na Airtel. Kushoto ni mmoja wa washindi hao, Dk Joseph Mambo wa Dar es Salaam na kulia ni Jane Matinde wa Airtel. Washindi hao walijishindia shs milioni moja kila mmoja.
Mmoja wa washindi 10 bora wa promosheni ya ‘Nani Mkali’ ya kampuni ya Airtel, Dk Joseph Mambo mkazi wa Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutangaza washindi kumi wa promosheni hiyo, jijini humo jana. Katikati ni Dangio Kaniki na Jane Matinde, Maofisa Uhusiano wa Airtel. Washindi hao walijishindia shs milioni moja kila mmoja.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia) akimpongeza mmoja wa washindi 10 bora wa promosheni ya ‘Nani Mkali’ inayoendeshwa na Airtel, Dk Joseph Mambo wa Dar es Salaam katika hafla ya kutangaza washindi hao jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Dangio Kaniki wa Airtel. Washindi hao walijishindia shs milioni moja kila mmoja.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewazawadia washindi kumi bora (bonus winners) wa promosheni ya Nani Mkali ambapo Kila mshindi amepata nafasi ya kujishindia pesa taslim shilingi milioni moja.

Airte imewazawadia leo wateja mbao wamekuwa wakishiriki promosheni hii mara nyingi toka ilipoanza, na washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Dar es Salaam, Njombe, Mbeya, Tanga, Tabora, Arusha na Lindi.

Akiongea wakati wa kuwatangaza washindi hao Afisa uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki alisema” leo tunayofuraha kuwatangaza washindi wa bora katika promosheni hii inayoendelea ya nani Mkali na kuwazawadia kwa kushiriki kikamilifu tunaoa amasa kwa wateja kujiunga na kushiriki.

Airtel bado inaendelea kuwapatia nafasi nyingine watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu, zaidi ya shilingi milioni 50 bado kushindaniwa na washindi wanaendelea kupatikana mpaka mwisho wa shindano hili mwezi huu. Katika promosheni hii wateja wanapata nafasi ya kujishindis shilingi million moja kila siku, million tatu kila wiki na kila mwezi”.

Washindi bora wa promosheni ya nani Mkali ni pamoja na:
Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Dangio

kujiunga na “Nani Mkali”, mteja anatakiwa kuandika neno “Mkali” na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad