HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 16, 2012

SSRA YAKUTANA NA WASTAAFU MKOA WA DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka akizungumza na wastaafu wa mkoa wa Dodoma (hawapo pichani).Wastaafu hao walikutana na uongozi wa Mamlaka ili kuelezea mafanikio na kero wanazokabiliana nazo katika malipo yao ya Pensheni.Wastaafu hao walimueleza mkurugenzi mkuu wa SSRA Bi.Irene Isaka kuwa Pensheni wanazolipwa ni ndogo sana ukilinganisha na hali halisi ya uchumi nchini.Wastaafu hao waliomba pensheni zipandishwe kulingana na thamani ya shilingi na pia sambamba na upandaji wa kima cha chini cha mshahara.Wastaafu waliipongeza Hazina kwa kutatua baadhi ya kero zao, kwani kero nyingi walizosiwasilisha katika kikao chao cha mwisho zimetatuliwa.Pia waliipongeza Serikali kupitia Wizara ya kazi na Ajira na waheshimiwa wabunge kwa kupitisha muswada wa mabadiliko ya sheria za mifuko ya hifadhi ya Jamii, kwani kwa kupitisha muswada huo wana imani kubwa kuwa Mamlaka imepewa meno nayo itafanya kazi kikamilifu na kuboresha pensheni,huduma na mafao yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya jamii.
Wastaafu wa mkoa wa dodoma wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa SSRA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wastaafu wa mkoa wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad