Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo na kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu,Marehemu Harun Mahundi aliyefariki Dunia april 5, 2012 na kuzikwa jana jijini Dar es salaam. Hapo ni nyumbani kwa marehemu Mikocheni barabara ya Rose Garden,jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji watoto wa Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu,Marehemu Harun Mahundi aliyefariki april 5, 2012 na kuzikwa jana jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na waombolezaji nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo alikofika kuomboleza nao msiba huo mkubwa kwa taifa letu kiujumla.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba,Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa,hapa akisalimianaa na mdogo wake na Marehemu Steven Kanumba.
Rais Kikwete akiwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo alikofika kuomboleza nao msiba huo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanakamati ya msiba wa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo alikofika kuomboleza nao kifo hicho.
Rais Kikwete akiaga waombolezaji nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam leo.
Rais Kikwete akiongea na waandishi wa habari wakati akiondoka msibani hapo.
It's true Steven Kanumba dies!!!I can't believe so!what happened to him? O my God,why?
ReplyDelete