HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 23, 2012

KERO YA WAKAZI WALIOKARIBU NA SOKO LA ILALA JUU YA WAFANYABIASHARA WA SOKO HILO

Ni muda wa saa 10 Jioni ya leo mitaa ya Ilala karibu na Soko la Ilala Boma ambapo kumekuwa na kero kubwa sana inayotupata wakazi wa eneo hili kila siku iendayo kwa Mungu.kama inavyoonekana pichani,hapa ni moja ya lori la mizigo likiwa limesimama katikati ya njia huku makuli wa sokoni hapo wakishusha magunia ya viazi na kuyapeleka sokoni.basi hapo ni mwendo wa makelele,fujo nk.

kiasi kwamba hata kama kukiwa na mgonjwa anaetaka kuwahishwa hospitali kwa haraka kupita inakuwa shida kwa sababu njia nzima imejaa magari na wafanya biashara wa sokoni hapo.

Mzee wa Mtaa kwa Mtaa tunaomba uliwasilishe jambo hili kwa wahusika kupitia libeneke lako pendwa ili waweze kulitafutia ufumbuzi wa haraka maana hii ni kero kubwa sana kwetu.

Mdau wa Mtaa kwa Mtaa
Mkazi wa Ilala Mtaa wa Nzasa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad